Mrisho Ngasa akifika Coco Beach kwa ajili ya mazoezi na timu yake mpya |
Ngasa akiwa mazoezini |
Richard Amatre |
Kocha msaidizi
wa klabu ya soka ya simba ya jijini dar es saam ambao ni mabingwa wa ligi kuu
soka tanzania bara richard amatre amemtaka mchezaji mpya wa timu hiyo
waliyemsajili kutoka kutoka klabu ya Azam FC Mrisho Khalifani Ngasa kujituma na
kudhihirisha kwamba yeye ni bora.
Kocha huyo ameyasema hayo
wakati wa mazoezi ya klabu hiyo yanayofanyika katika fukwe za coco beach jijini
dar es salaam.
Amatre ambaye ni raia
wa uganda amesema ngasa ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa sana wa
kusakata kabumbu , hivyo anatakiwa kutilia makazao mazoezi kuhakish
a anajituma kwa maslahi ya timu yake ya simba ili kuondoa dhana iliyojengeka
katika vichwani mwa watu kwamba ana mapenzi zaidi na mahasimu wa klabu hiyo
klabu ya yanga ya jijini dar es salaam.
Klabu ya soka ya azam fc ilifkia uamuzi wa
kumuuza mchezaji huyo kufuatia uamuzi wa mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake
ya zamani ya yanga katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la kagame
iliyozikutanisha timu za Azam FC na AS Vita ya kutoka Jamhuri ya kidemokrasia
ya kongo.
No comments:
Post a Comment