Wednesday, July 18, 2012

ATLETICO NA TUSKER WATAMBA KUTWAA UBINGWA WA KOMBE LA KAGAME

Kaze Cedri - Kocha wa Atletico
Makocha wa timu za Tusker na Atletico zinazoshiriki michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati Kagame wamesema ukiondoa timu za EL salaam Wau ya Sudan na Ports ya Djibout timu zilizobakia yeyote inaweza kutwaa kombe hilo.

Makocha hao ambao ni Kaze Cedrio wa Atletico ya Burundi na Sam Omolo wa timu ya Tusker kutoka nchini Kenya wamesema hayo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha Cedrio ameongeza kuwa licha ya kuwa timu nyingi zimejiandaa vema lakini wachezaji wake wakijitahidi na kufuata maelekezo anayoyaeleza ana imani mwaka huu kombe hilo litaenda nchini Burundi.

Sam Omolo –kocha mkuu wa Tusker
Kwa upande wake kocha Sam amebainisha kuwa timu zimejiandaa vizuri lakini timu itafanya vizuri maana ni timu nzuri na pia itaonyesha changamoto.

Jumla ya timu 11 zimeshiriki michuano hiyo kutoka ukanda wa Afrika ,Mashariki na kati CECAFA ambapo inafanyika kwa mara ya pili mfululizo nchini Tanzania huku Yanga ikiwa ni Bingwa mtetezi wa kombe hilo.




No comments:

Post a Comment