Monday, July 16, 2012

YUSUF MANJI, MWENYEKITI MPYA WA YANGA



Manji na Wanayanga (Picha Kandanda.co.tz)
Hatimaye wanachama wa timu ya soka ya Yanga wamepiga kura na kumchagua aliyekuwa mfadhili wa zamani wa timu hiyo bwana Yusuf Manji kuwa mwenyekiti wa timu. Uchaguzi huo ambao ulifuatiwa na vurugu nyingi majira ya saa nane za usiku baada ya matokeo kuchelewa kutangazwa ulifanyika jana katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Lakini walinzi walituliza vurugu hizo mpaka hapo kura za mwenyekiti zilipohesabiwa.



Manji ameibuka mshindi dhidi ya wagombea wengine Joel Jembele na Edgar Chibura. Uchaguzi huo umefuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo ya wanajangwani Lloyd Nchunga na makamu wake Davies Mosha pamoja na wajumbe kadhaa.

No comments:

Post a Comment