Shirikisho la ngumi za ridhaa tanzania BFT limeitaka mikoa
kuchagua mabondia wenye viwango watakaoshiriki mashindano ya ubingwa taifa
yanatarajiwa kuanza agosti 25 hadi 30 mwaka huu jijini dar es salaam.
Katibu mkuu wa BFT makore mashaga amesema kila mkoa unatakiwa
kutafuta bingwa ambaye atakidhi viwango na kwamba ni vyema viongozi waliopewa
jukumu la kuchagua mabingwa waangalie vigezo vinavyostahili.
Mashaga amesema ili timu ya taifa iweze kupata mabondia wazuri
ni lazima viongozi waangalie uwezo wa wachezaji ambao watakuja kuliwakilisha
vema taifa katika mashindano ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment