Friday, July 20, 2012

YONDANI RUHUSA KUCHEZEA YANGA

Kevin Yondani
Sakata la  aliyekuwa mchezaji wa timu ya soka ya Simba  Kelvin Yondani  limechukua sura mpya ambapo sasa kamati ya sheria maadili, na hadhi za wachezaji  imeweka bayana uhalali wa kuichezea timu ya soka ya Yanga msimu ujao wa ligi.

Ni katika ofisi za Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF ambapo maamuzi hayo yametolewa na kamati hiyo baada ya malumbano ya siku kadhaa kati ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini  Angetile Oseah na Uongozi wa klabu ya soka ya Simba ya Dar es Slaam

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kamati hiyo Alex Mgongolwa amesema kamati ilikutana kwenye ofisi za  (TFF) julai 17 mwaka huu baada ya kupitia mikataba na nyaraka mbali mbali  za mchezaji huyo ilibaini mchezaji huyo hana hatia na halali kutinga  mitaa ya Twiga na jangwani na hata kuichezea timu hiyo katika kichuano ya komba la Kagame

Amesema kwa mujibu wa mapatio ya nyaraka hizo kamati iliridhika na suala la yondani na kudai kuwa ni la kiutendaji, ambapo maamuzi ya sekretarieti kuwasiliana na klabu ya Simba kwa madai ya suala hilo kama skretarieti hiyo ilivyofanya katika barua yake ya julai 14 mwaka huu yalikuwa ni sahihi.

Amesema kuwa kamati imebaini mkataba wa mchezaji huyo na klabu ya Simba ulimalizika  mei 31 mwaka huu hivyo kwa taratibu za usajili wake nyota huyo alikuwa huru  kuichezea timu yoyote kuanzia juni mosi mwaka huu.

Aidha amesema kuwa mkataba wa Mchezaji huyo uliowasilishwa TFF juni 6 mwaka huu na klabu hiyo  ikiwa na lengo la kuuongeza ilikwenda kinyume na sheria za utaratibu wa usajili.

Amesema mkataba huo ulionekana kuwa na mapungufu ya kisheria hususani katika tarehe ambazo pande  zote  mbili ziliingia makubaliano hayo, na kusema mkataba huo umebainisha yondani alisaini mkataba desemba 23 mwaka 2012 na klabu ya simba kupitia kwa makamu Mwenyekiti wake Godfrey Nyange Kaburu.

Mchezaji huyo alisajiliwa na klabu ya Yanga msimu huu akitokea klabu ya Simba ambapo usajili wake  ulileta  utata miongoni mwa timu hizo kongwa nchini.
MWISHO.

No comments:

Post a Comment