Boniface Wambura |
Baraza la vyama vya mpira
wa miguu afrika mashariki na kati CECAFA
limefanya mabadiliko madogo katika
ratiba yake ya michuano ya komba la kagame kwa kurudisha nyuma mchezo kati ya
timu ya soka ya simba na URA ya Uganda.
Akizungumza jijini dar es
salaam Ofisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Boniface Wambura amesema
kuwa mchezo huo sasa utafanyika jumapili ya julai 15 katika uwanja wa taifa
badala ya jumatatu ya julai 16 mwaka huu.
CECAFA limefanya mabadiliko hayo kutokana na fainali ya Copa Coca-Cola 2012
iliyokuwa ichezwe kwenye uwanja huo kuhamishiwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mechi ya Simba na URA ya Uganda kuwania Klabu bingwa Afrika
Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) iliyokuwa ichezwe Jumatatu (Julai 16 mwaka
huu) sasa itafanyika Jumapili (Julai 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
CECAFA limefanya mabadiliko hayo kutokana na fainali ya Copa Coca-Cola 2012
iliyokuwa ichezwe kwenye uwanja huo kuhamishiwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Kutokana na mabadiliko hayo, mbali ya mechi ya Simba na URA
itakayoanza saa 10 kamili jioni, mechi nyingine Jumapili itakuwa kati ya Vita
Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) dhidi ya Ports ya Djibouti
itachezwa saa 8 kamili mchana Uwanja wa Chamazi.
Pia siku hiyo hiyo ya Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi kutakuwa
na mechi nyingine itakayoanza saa 10 kamili jioni. Mechi hiyo itazikutanisha
timu za Azam ya Tanzania Bara na Mafunzo kutoka Zanzibar.
Mechi za ufunguzi wa
mashindano hayo Jumamosi (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam zitabaki kama zilivyopangwa awali. Mechi ya kwanza saa 8 mchana itakuwa
kati ya APR ya Rwanda na El Salam Wau ya Sudan Kusini wakati saa 10 kamili
jioni Yanga itaoneshana kazi na Atletico ya Burundi.
No comments:
Post a Comment