Alfonce Mchumiatumbo |
Bingwa wa ngumi za kulipwa za uzito wa juu hapa nchini
Alfonce Mchumia Tumbo amesema yupo tayari kupambana na Awadhi Tamimu muda
wowote na sehemu yeyote endapo atatokea promota wa kuandaa pambano hilo.
Bondia huyo anayeinukia hivi sasa katika masumbwi ameibuka
na tambo hizo baada ya tetesi kuwa
Tamimu amekosa mpinzani wa kupambana nae ili kutetea mikanda anayoishikilia.
Mchumia tumbo ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa
akikimbiwa na baadhi ya mabondia pamoja na kusaini makubaliano ya kupambana nae
amesema kwa sasa haoni bondia mwenye
uwezo wa kupanda nae ulingoni zaidi ya
Awadhi Tamimu ambaye kwa sasa anaishi Sweden.
Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wa habari
Mchumia Tumbo ameitaka kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC kuandaa
haraka iwezekanavyo pambano hilo ili aweze kumvua Tamimu mikanda yote ya uzito
wa juu anayoishikili.
Alfonce Mchumia Tumbo ambaye ni mzaliwa wa mkoani Mbeya anashika nafasi ya kwanza Tanzania na kwa viwango vya dunia nafasi ya
317 amepanda ulingoni mara 7 ameshinda mapambano 6 yote kwa KO ametoka sare
mchezo mmoja na hajapoteza pambano lolote.
Na Hassan Mvula
No comments:
Post a Comment