Thursday, July 26, 2012

YANGA NA AZAM KUKUTANA FAINALI KOMBE LA KAGAME

Timu za Azam FC na Yanga zimeingia katika fainali za kombe la Kagame ambapo watapambana katika mchezo wa kufa na kupona hapo jumamosi Julai 28 mwaka huu.

Azam mapema leo katika uwanja wa taifa Dar es Salaam, wameifunga timu alikwa ya AS Vita 2-1 baada ya Mrisho Ngasa kupachika goli la ushindi. Katika mchezo wa pili uliochezwa uwanja huo huo Yanga imeifunga APR ya Rwanda goli 1-0 katika dakika za nyongeza mnamo dakika ya 100. Goli hilo ambalo liliingizwa kimyani na Hamis Kiiza limewapa Yanga nafasi ya kukutana Azam katika fainali hizo.

AS Vita na APR watakutana siku ya Jumamosi pia kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wanayo kazi kubwa kutetea kombe hilo lisiende mikononi mwa wanalambalamba. Hata hivyo timu ya Azam FC imeonyesha kiwango kikubwa toka kwanzia msimu wa ligi kuu uliopita mpaka mashindano haya ya klabu bingwa za Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

No comments:

Post a Comment