Sunday, July 15, 2012

SIMBA APATA KIPIGO CHA 2 KAVU TOKA URA

Felix Sunzu (jezi namba 9) katika mpambano
Baada ya mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame Yanga kuchapwa 2-0 na Atletico ya Burundi juzi, jana mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Simba wamepokea kipigo cha 2-0 kutoka timu ya  Mapato ya Uganda (URA).

Kupitia mchezaji Owen Kasuule URA ilipata goli la kwanza mnamo dakika ya 11 na baadae kuongeza la pili manamo dakika ya 90 kupitia mchezaji Feni Ally. Simba ilijitahidi kucheza vizuri lakini haikufanikiwa kuliona lango la URA hadi mwisho wa mchezo.

Wakati huo huo Azam FC katika uwanja wa Chamazi complex ilitoka sare ya 1-1 na Mafunzo. Kabla ya mchezo huo Vita Club ya DRC iliipa kipigo cha mbwa Port of Djibuti na kuifunga magoli 7-0.

No comments:

Post a Comment