Saturday, July 21, 2012

SIMBA, AS VITA WATOKA SARE YA 1-1

Timu za Simba na AS Vita ya DRC zimetoka sare ya 1-1 katika mechi za mwisho za makundi na kuingia robo fainali za michuano ya kombe la Kagame. Vita ilijipatia goli la penati mapema na baadaye Haruna Moshi kusawazisha. Hata hivyo Simba walipata nafasi ya kushinda mnamo dakika za mwisho walipopata penati iliyopigwa na Felix Sunzu ambaye alikosa.

Mapema leo Azam FC na Tusker ya Kenya pia walitoka sare ya bila kufungana na kupelekea Tusker kung'olewa katika mashindano hayo pamoja na WAU El Salaam ya Sudan Kusini na Ports ya Djibuti.

Timu zilizofuzu kuingia robo fainali ni Yanga, URA, APR, Simba, Azam FC, Mafunzo, As Vita na Atletico

No comments:

Post a Comment