Chama cha netiboli nchini CHANETA kimezitaka timu mbalimbali
zitakazoshiriki mashindano ya ligi daraja la kwanza kurudisha fomu za kushiriki
ligi hiyo inayotarajiwa kuanza septemba 8 mwaka huu mjini Mbeya.
Kaimu katibu mkuu wa CHANETA Rose Mkisi amesema kuwa fomu hizo
zinatakiwa kurudishwa kabla ya julai 30 mwaka huu ili kuwezesha kamati ya
mashindano kukamilisha mapema mipango ya michuano hiyo.
Michuano hiyo inatarajiwa kushirikisha jumla ya timu 20 kutoka Tanzania bara na visiwani.
No comments:
Post a Comment