Monday, July 23, 2012

SIMBA ATAENDELEZA UBABE KWA AZAM?


Timu za Simba sports Clib na Azam Fc zote za jiijin Dar es salaam zinatarajiwa kushuka dimbani jumanne ya July 24 ikiwa na robo fainali ya nne ya kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na kati. Robo fainali nyingine itazikutanisha timu ya Atletico ya Burundi na timu ya As Vita kutoka nchini DRC.
 
July 12 mwaka huu timu za Simba na Azam zilikutana katika uwanja huo huo wa Taifa ikiwa na hatua ya fainali ya kombe la ujirani mwema na hatimaye timu ya Simba kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya Penalti na kuutwaa ubingwa.
 
Swali linabaki kwa mashabiki wa soka wa Tanzania Je Simba itaendeleza ubabe wake kwa timu hiyo ambayo imeoenekana kuwa na kiwango kizuri cha soka yenye maskani yao Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
 
Kunoga kwa mechi hiyo ni kuwa Timu hizo za Simba na Azam ndio wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya Afrika ambapo Simba itawakilishwa kwenye kombe la klabu Bingwa Barani Afrika wakati Azam wao wakijivinjari kwenye kombe la shirikjisho barani humo ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano hayo.
 
Katika michuano hii ya kombe la Kagame timu ya Simba imecheza mechi tatu, na kushinda mechi moja, kutoka sare moja na kufungwa mchezo mmoja wakati Azam wao wamecheza michezo miwili na kutoka sare michezo yote.

Nao Atletico ya Burundi waliopewa jina na watemi wa Yanga watajitupa uwanjani kuikabili timu ya AS Vita kutoka Congo ambao ni wageni waalikwa wa kombe hilo mchezo utakaonza saa nane mchana na kufuatiwa na Mchezo Simba na Azam ambao ndio shauku kubwa ya wapenzi wa soka nchini.

Baada ya kukutana jumanne hii timu za Simba na Azam zitakutana mapema Septemba mwaka huu kwenye kombe la ngao ya Hisani baada ya timu ya Simba kumaliza bingwa kwenye ligi kuu soka Tanzania bara wakati Azam wakishika nafasi ya pili.


No comments:

Post a Comment