Saturday, July 14, 2012

WANAYANGA WAOMBWA KUJITOKEZA KWA AJILI YA UCHAGUZI


Makao makuu ya klabu ya Yanga Dar es Salaam

KUFUATIA uchaguzi wa viongozi wa klabu ya Yanga unatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam uongozi wa yanga na wanachama wa matawi mbali mbali kutoka Tanzania bara na Visiwani wametoa maoni  yao kuhusu uchaguzi huo.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenykiti wa klabu hiyo Lyoid Nchunga na makamu wake Davis Mosha na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendandaji wa Yanga.
Selestine Mwesigwa - Katibu Mkuu Yanga

Katibu mkuu wa klabu hiyo Selestine Mwasigwa amewataka wanachama wa klabu ya Yanga kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo na kuchagua viongozi wanaofaa kuongoza klabu hiyo.

Wakati huu timu ya Yanga imefunguwa mashindano ya CECAFA Kombe la Kagame kwa kuchuana vikali na timu ya Atletico ya Burundi. Mpaka sasa kipindi cha pili dakika ya 85 timu ya Atletico imefunga goli moja na Yanga haijapata kuziona nyavu za Atletico

No comments:

Post a Comment