Saturday, July 28, 2012

YANGA ATETEA UBINGWA WA KOMBE LA KAGAME

Hamis Kiiza akishangilia goli lake
Mabingwa wa tetezi wa kombe la Kagame la CECAFA Young Africans ya jijini Dar es Salaam wametetea ubingiwa huo mbele ya timu ya Azam FC katika mchezo wa fainali uliomalizika hivi punde katika uwanja wa taifa jijini hapa.

Ushindi huo wa kusisimua umefikiwa baada ya Hamis Kiiza na Said Bahanuzi kufumania nyavu za wanalambalamba hao kutoka Chamazi. Kiiza alifunga bao la kwanza kipindi cha kwanza na dakika ya 90 Baanuzi alishindilia msumari wa mwisho na kuongeza shangwe za ushindi wa goli mbili bila.

Michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda ilishirikisha timu jumla ya timu 11 ikiwemo AS Vita iliyoingia kama timu alikwa na kushinda nafasi ya mshindi wa 3 katika mechi waliyochezwa mapema leo na APR ya Rwanda. Jumla ya dola za kimarekani 60,000 zilikuwa zikigombewa katika mashindano hayo.

Mwaka jana Yanga iliibuka mshindi katika fainali iliyochezwa uwanja wa taifa dhidi ya Simba Sports Club.

No comments:

Post a Comment