Showing posts with label Kombe la ujirani mwema 2012. Show all posts
Showing posts with label Kombe la ujirani mwema 2012. Show all posts

Friday, July 13, 2012

SIMBA YATWAA KOMBE LA UJIRANI KWA MIKWAJU YA PENATI


Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi kwa kumbeba kipa wa mahiri Juma Kaseja baada ya kutwaa ubingwa zidi ya timu ya Azam FC jana katika uwanja wa Taifa

Kapten wa timu ya Simba akipokea kombe kutoka kwa Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar Mh. Machano Othman Said.

Timu hizo zilifungana 2-2 dakika 90 za kwanza na hivyo kupelekea mechi hiyo kufika kwenye mikwaju ya penati ambapo Simba walipata 4 na Azam 2. Hivyo hadi mwisho wa mchezo Simba alishinda 6-4.

Thursday, July 12, 2012

SIMBA NA AZAM KUUMANA LEO TAIFA





Mabingwa wa soka tanzania bara timu ya soka ya Simba hii leo inashuka dimbani kupambana na timu ya soka ya Azam fc katika pambano litakalofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Katika pambano hilo linalotarajia kuanza majira ya saa moja kamili ni la fainali ya kombe la ujirani mwema ambapo katika hatua za awali michuano hiyo ilifanyika katika uwanja wa amani zanzibar.
Msemaji wa shirikisho la soka nchini TFF boniface wambura amesema kuwa mchezo huo umepangwa kuchezwa muda huo kutokana na kutoa nafasi kwa mashabiki wengi wa mchezo huo kuweza kuhudhuria kwa wingi