Saturday, August 4, 2012

NGASA ATAKIWA KUJITUMA KUONYESHA KUWA YEYE NI BORA

Mrisho Ngasa akifika Coco Beach kwa ajili ya mazoezi na timu yake mpya

Ngasa akiwa mazoezini

Richard Amatre

Kocha msaidizi  wa klabu ya soka ya simba ya jijini dar es saam ambao ni mabingwa wa ligi kuu soka tanzania bara richard amatre  amemtaka mchezaji mpya wa timu hiyo waliyemsajili kutoka kutoka klabu ya Azam FC Mrisho Khalifani Ngasa kujituma na kudhihirisha kwamba yeye ni bora.

Kocha huyo ameyasema hayo wakati wa mazoezi ya klabu hiyo yanayofanyika katika fukwe za coco beach jijini dar es salaam. 

Amatre ambaye ni raia wa uganda amesema ngasa ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa sana wa kusakata kabumbu , hivyo  anatakiwa  kutilia makazao mazoezi kuhakish a anajituma kwa maslahi ya timu yake ya simba ili kuondoa dhana iliyojengeka katika vichwani mwa watu kwamba ana mapenzi zaidi na mahasimu wa klabu hiyo klabu ya yanga ya jijini dar es salaam.

Klabu ya soka ya azam fc ilifkia uamuzi wa kumuuza mchezaji huyo kufuatia uamuzi wa mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani ya yanga  katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la kagame iliyozikutanisha timu za Azam FC na AS Vita ya kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo.

Friday, August 3, 2012

HATIMAYE NGASA ATINGA UZI WA MSIMBAZI

Mrisho Ngasa baada ya mazoezi
 
Hatimaye yametimia. Mrisho Ngassa tayari ameshajiunga rasmi na kambi ya timu ya Simba na kukabidhiwa uzi mwekundu huku namba yake nyuma ya jezi ikisomeka 16. Leo ameanza amehudhuria mazoezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza katika ufukwe wa coco beach na pia ametambulishwa rasmi makao makuu ya Klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kukabidhiwa mchuma mpya

Saturday, July 28, 2012

YANGA ATETEA UBINGWA WA KOMBE LA KAGAME

Hamis Kiiza akishangilia goli lake
Mabingwa wa tetezi wa kombe la Kagame la CECAFA Young Africans ya jijini Dar es Salaam wametetea ubingiwa huo mbele ya timu ya Azam FC katika mchezo wa fainali uliomalizika hivi punde katika uwanja wa taifa jijini hapa.

Ushindi huo wa kusisimua umefikiwa baada ya Hamis Kiiza na Said Bahanuzi kufumania nyavu za wanalambalamba hao kutoka Chamazi. Kiiza alifunga bao la kwanza kipindi cha kwanza na dakika ya 90 Baanuzi alishindilia msumari wa mwisho na kuongeza shangwe za ushindi wa goli mbili bila.

Michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda ilishirikisha timu jumla ya timu 11 ikiwemo AS Vita iliyoingia kama timu alikwa na kushinda nafasi ya mshindi wa 3 katika mechi waliyochezwa mapema leo na APR ya Rwanda. Jumla ya dola za kimarekani 60,000 zilikuwa zikigombewa katika mashindano hayo.

Mwaka jana Yanga iliibuka mshindi katika fainali iliyochezwa uwanja wa taifa dhidi ya Simba Sports Club.

MATARAJIO YA WATANZANIA OLYMPIC 2012

Washiriki wa Olympic kutoka Tanzania
Baadhi ya waandishi waandamizi wa habari  wa michezo nchini wameoenyesha wasiwasi wa kufanya vema kwa wanamichezo kutoka nchini wanaoshiriki michuano ya olimpiki inayoendelea jijini London kutokana na maandalizi yasiyokuwa endelevu kwa wanamichezo mbalimbali.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 204 zinazoshiriki mashindano hayo makubwa zaidi dunuiani katika michezo ya Ngumi Kuogelea na Riadha.

Ni katika hafla ya fupi ya kusheherekea kuanza kwa michuano hiyo iliyowakutanisha baadhi ya waandishi wa habari za michezo bega kwa bega na futari iliyondaliwa na kampuni ya Multchoice Tanzania kwa waandishi wa habari za michezo nchini ndipo suala la kutokuwa na imani na timu hiyo lilipoibuka.

Nao baadhi ya waandishi wa habari za michezo wamekuwa na maoni  tofauti, wapo wanaoamini kuwa wanamichezo hao watafanya vema huku wengine wakiweka bayana kamwe medali haziwezi kupatikana kutokana na aina ya maandalizi yaliyofanyika.

Aidha kwa upande wake Barbara Kambogi, Afisa habari wa Multichoice ametoa rai kwa watanzania kuwapa nafasi wanamichezo hao kwa kuamin kuwa watafanya vema.
 
Katika mchezo wa Ngumi Tanzania inawakilishwa na Suleiman Kidunda anayepigana Uzito kilo 64, Zakia Mrisho anayekimbia Riadha mita 1, 500, Msenduki Mohamed, Faustine Mussa, Samson Ramdhani wao watakimbia riadha nusu marathoni yaani kilomita 21.
 

Friday, July 27, 2012

MCHUMIA TUMBO AJITOKEZA KUPAMBANA NA AWADHI TAMIMU




Alfonce Mchumiatumbo


Bingwa wa ngumi za kulipwa za uzito wa juu hapa nchini Alfonce Mchumia Tumbo amesema yupo tayari kupambana na Awadhi Tamimu muda wowote na sehemu yeyote endapo atatokea promota wa kuandaa pambano hilo.

Bondia huyo anayeinukia hivi sasa katika masumbwi ameibuka na tambo hizo baada ya   tetesi kuwa Tamimu amekosa mpinzani wa kupambana nae ili kutetea mikanda anayoishikilia.

Mchumia tumbo ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa akikimbiwa na baadhi ya mabondia pamoja na kusaini makubaliano ya kupambana nae amesema kwa sasa haoni  bondia mwenye uwezo wa kupanda nae ulingoni  zaidi ya Awadhi Tamimu ambaye kwa sasa anaishi Sweden.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wa habari Mchumia Tumbo ameitaka kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC kuandaa haraka iwezekanavyo pambano hilo ili aweze kumvua Tamimu mikanda yote ya uzito wa juu anayoishikili.

Alfonce Mchumia Tumbo ambaye ni mzaliwa wa mkoani Mbeya anashika nafasi ya kwanza Tanzania na kwa viwango vya dunia nafasi ya 317 amepanda ulingoni mara 7 ameshinda mapambano 6 yote kwa KO ametoka sare mchezo mmoja na hajapoteza pambano lolote.

Na Hassan Mvula

Thursday, July 26, 2012

YANGA NA AZAM KUKUTANA FAINALI KOMBE LA KAGAME

Timu za Azam FC na Yanga zimeingia katika fainali za kombe la Kagame ambapo watapambana katika mchezo wa kufa na kupona hapo jumamosi Julai 28 mwaka huu.

Azam mapema leo katika uwanja wa taifa Dar es Salaam, wameifunga timu alikwa ya AS Vita 2-1 baada ya Mrisho Ngasa kupachika goli la ushindi. Katika mchezo wa pili uliochezwa uwanja huo huo Yanga imeifunga APR ya Rwanda goli 1-0 katika dakika za nyongeza mnamo dakika ya 100. Goli hilo ambalo liliingizwa kimyani na Hamis Kiiza limewapa Yanga nafasi ya kukutana Azam katika fainali hizo.

AS Vita na APR watakutana siku ya Jumamosi pia kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wanayo kazi kubwa kutetea kombe hilo lisiende mikononi mwa wanalambalamba. Hata hivyo timu ya Azam FC imeonyesha kiwango kikubwa toka kwanzia msimu wa ligi kuu uliopita mpaka mashindano haya ya klabu bingwa za Afrika Mashariki na Kati CECAFA.